Menu
RSS
Afya

Lishe bora tiba ya utapiamlo.

Lishe bora tiba ya utapiamlo

Na Mwandishi Wetu

Hali ya afya na lishe bora kwa mama mjamzito ni muhimu kabla na baada ya ujauzito kwa kuwa husaidia kuwepo kwa matokeo mazuri ya ujauzito na kufanikisha unyonyeshaji wa maziwa ya mama.

Ndani ya siku 1000 yani tangu mama apate ujauzito hadi mtoto anapofikisha umri wa miaka miwili  ni muhimu akazingatia lishe bora pamoja na mtoto wake ili kuhakikisha mtoto anakua vizuri na kuepuka matatizo ambayo anaweza kuyapata ikiwemo utapiamlo, ugonjwa unaotokana na kupunguza au kuzidisha mahitsaji muhimu katika mwili.

Kuna aina mbalimbali za utapiamlo ambazo mtoto anaweza kuzipata ikiwemo utapiamlo wa kukonda, utapiamlo wa ufupi na hali hiyo huwa hivyo mpaka kwenye maendeleo ya ubongo wake.

Mtoto kuwa na uzito usioendana na  umri na utapiamlo wa madini na vitamini ambao unaweza kuwapata hata watoto warefu  na kwamba una dumaza ubongo wa mtoto.

“Unaweza kumkuta mtu mrefu lakini amekuwa na shida katika uelewa wake kwakuwa anakuwa na uelewa wa hali ya chini sana”,anasema Mary.

Utapiamlo usababishwa na mambo mbalimbali ikiwemo  ukosefu wa chakula, hali ya usafi wa chakula, kutokuwepo kwa uangalizi na kwamba zipo sababu zilizojificha ambazo ni pamoja na umaskini unaobabisha kukosa chakula, uwezo wa mama kufanya maamuzi na mazingira ya njaa na hivyo waathirika wakuu ni watoto walio chini ya umri wa miaka miwili na kina mama.

Mary alieleza kuwa madhara ya utapiamlo kuwa ni pamoja na vifo vya watoto 130 kila siku, huaribu mfumo wa kinga mwili na kusababisha maradhi, watoto waliozaliwa na uzito pungufu hupata kisukari, hupata matatizo ya moyo, kuwa na uwezo mdogo na kukosa  uwezo wa kuzalisha na kufanya maamuzi.

Binafsi nimeshuhudia baadhi ya watoto waliopata utapiamlo kutokana na kutozingatia taratibu za lishe ambazo mzazi ama mlezi anatakiwa kuzifuata ikiwa pamoja na wazazi wenyewe kuwa na afya duni,  hali inayoweza kusababishwa na mambo mbalimbali yanayomkwamisha mama kupata lishe bora kwake na mtoto wake.

Mary Kabona Mtaalamu wa lishe kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni katika semina ya waandishi wa habari kuhusu Lishe ya watoto na maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji ambayo ufanyika kila mwaka Agosti Mosi hadi Agosti 7, alisema kuwa ikiwa mama mjamzito atakosa lishe bora hata mtoto wake atapata utapiamlo.

“Licha ya mtoto kupata utapiamlo hali hiyo uweza kusababisha kifo kuzorotesha maendeleo ya mtoto, Udhoofisha ubongo wa mtoto na ingawa mtoto anakuwa mtu  lakini si mtu bora yaani ni  mtu asiye na uwezo’’,anasema Mary. 

Mary anaeleza kuwa hali ya lishe na ulishaji watoto wachanga nchini Tanzania si ya kuridhisha kwa kuwa wazazi au walezi wanashindwa kuzingatia taratibu za lishe kwa watoto wao wawapo wa changa hali inayosababisha asilimia kubwa ya wazazi kukiuka taratibu za kiafya kwa kuwapatia watoto chakula cha nyongeza kabla ya wakati unaotakiwa kitalaam.

“Hali ya lishe kwa watoto nchini si nzuri  kwani takwimu za mwaka 2010 zinaoonesha 42% ya watoto wanatatizo la udumavu, utapiamlo  huku mwaka jana  2014hali hiyo ilionekana kushuka na kufikia 34.7%, na kwamba kitaifa tupo katika hali ya juu ya tatizo ingawa  mikoa mingi iliyo na tatizo la utapimlo ina chakula cha kutosha’’,anasema Mary.

Mary anadokeza kuwa  kuwepo kwa tatizo la utapiamlo katika mikoa iliyo na chakula cha kutosha kunatokana na aina ya ulishaji watoto isiyozingatia kanuni na taratibu za afya katika suala la ulishaji watoto ikiwa ni pamoja kumpa mtoto chakula cha aina moja, mama aliyejifungua kutomnyonyesha mtoto mapema  ndani ya saa moja.

Nyingine ni pamoja na mama kumpa mtoto maziwa ya njano mapema kwa kuwa yana kinga mwili nyingi na vitamin A,kutokumnyonyesha usiku na mchana  kila wakati miezi sita  bila kumpa kitu kingine kwa kuzingatia taratibu za afya.

 Anasema kuwa  matumizi ya chupa ya maziwa kwa mtoto mdogo ni hatari  kwani hayastahili, aliongeza kuwa  na takwimu za mwaka 2010 kwa wazazi wanaozingatia taratibu za ulishaji watoto nchini kuwa ni 49% na hadi kufikia mwaka 2014  imefikia 50.8% na hu8ku nusu ya watoto wakionekana  kucheleweshwa.

Taratibu zinazokiukwa kuwa ni pamoja na kuwapa watoto chakula cha nyongeza mapema kabla ya kufikisha miezi sita, hali inayohatarisha afya ya mtoto, kutokana na kumpa vitu vinavyohatarisha afya yake.

Ukiukwaji mwingine unaofanywa na wazazi na walezi ni 5% ya watoto walio chini ya miezi sita wanapewa  maziwa yasiyo ya mama na wqengine wakiwapa maziwa ya chupa.

Mary anaeleza kuwa hata wakati wa ulishaji vyakula vya nyongeza  asilimia 24ya wazazi ndio wanaowapa watoto wao chakula chenye mchanganyiko unaotakiw, angalau kiwe na maziwa ikiwa pamoja na kuzingatia umri wake ambapo ni asilimia 20ya  wazazi ndio   wanaozingatia hilo kwa watoto wao.

Aidha Mary alidokeza kuwa ukiukwaji wa taratibu za ulishaji mtoto zinatokana na changamoto mbalimbali ambazo ni pamoja na  kutokuwepo kwa rasilimali watu na rawsilimali fedha,  tafiti zinazofanyika kuhusu suala hilo ni ndogo,   Sheria ya mateniti kutotekelezwa  lakini pia uuzaji wa chakula cha mtoto kinyume na taratibu za afya.

Nyingine ni mabadiliko ya tabia nchi,majanga ya wakimbizi, mabovu, mafuriko yanayowaathiri mama na mtoto, upungufu wa kinga mwilini HIV ambapo mtoto akipata maaambukizi afya yavke inakuwa mgogoro.

“Lakini hata wakina mama kuwa busy na kazi hali inayosababisha watoto kushindwa kunyonya vizuri ni moja ya changamoto inayochangia wazazi kushindwa kufuata utaratibu wa afyas katika malezi ya watoto na kusababisha changamoto za kiafya kwa watoto wao.

Binafsi naamini hakuna linaloshindikana chini ya jua ni kiasi cha kuamua na kuchukua hatua ili kuwasaidia watoto kukua vizuri kimwili na kiakili ikiwa pamoja na kuhakikisha Taifa linaendelea kwani udumavu kwa watoto unarudisha nyuma maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.

Ni wakati sasa wa wanawake kuamka na kufuata taratibu za kiafya zinazotolewa na wataalam wa afya ili kuwapa watoto wadogko au wachanga kinachostahili  ikiwa ni njia bora ya kuepuka tatizo la udumavu linalowakuta watoto wengi nchini na kusababisha kurudisha nyuma maendeleo yao ya kimwili na kiakili, kumaliza tatizo la udumavu nchini inawezekana.

Read more...

Lishe bora bado mwiba kwa watoto Tanzania

Na Celina Joseph                   

Imeelezwakuwawatoto 42 katika ya 100 nchini Tanzania wanaudumavukutokananakukosalishe bora. 

Hayoyalielezwa hivi karibuni na  Lediana Mngong’o, Mwenyekitikikundi cha Wabunge wa masualayalishe uhakikawachakulanahakizawatoto,katikauzinduziwaripotiyaKimataifayalishe iliyofanyikakatika Hotel yaProteajijini Dar esSalaam. 

Alisema hali ya duni ya lishe inaathari kubwa  hasa katika siku 1000 za mtoto tangu kutungwa mimba,kuzaliwa hadi anapofikisha miaka miwili na kwamba tatizo hilo endapo litaendelea mtoto anaweza kudumaa kiakili na humuathiri mtoto katika maisha yake yote.

Alisema lishe bora ni muhimu kwa mtoto hivyo elimu inatakiwa kutolewa kwa akinamama kuwanyonyesha watoto wao maziwa ya mama pekee bila kuwapa vyakula hadi wanapofikisha umri wa miezi sita.

Alisema licha ya kuwa suala hilonchininimtambuka linahitaji  juhudinauwajibikaji  kwakilammojaikiwemoserikali, sekta binafsi kuwekeza katika lishenavyombovyahabariambaowanawezakutoaelimukwajamii. 

Kwa upande wake MratibuwaLisheOfisiyaWaziriMkuu Saraha Mshiu, alisema Tanzania kwakiasifulani imepigahatuakatikakupunguzatatizo la lishekutokaasilimia 42 hadi 37.5 ndani ya  miaka mitano iliyopita.

Alisema bado tatizo la lishe bora linatakiwa kupewa kipaumbele na kuongeza kuwa Serikali imejipanga kutoa elimu zaidi ya suala hilo na madhara ya ukosefu wa lishe bora na udumavu.

Alisema Serikali pia imejipanga kushirikisha sekta binafsi kuwekeza katika suala la lishe bora na kutoa nafasi kwa taasisi hizo kuwaruhusu akinamama waliojifungua kuwanyonyesha watoto wao kwa kipindi cha miezi sita mfululizo ndipo arejee kazini kwani kufanya hivyo watapunguza utapia mlo na udumavu.

Alisema kwa kuwa serikali inalitambua suala la lishe kuwa ni mtambuka  mwakajanailizinduampangowakuongezaviinilishekatikavyakulaikiwanipamojanaungawanganonamafutayakulaambayo yanatumiwa na kila hadi vijijini. 

Naye Lyidia Bendera KatibuMkuu  waChamaChaADC  alisemaSerikaliitakayoingiamadarakanikwadhamanayamiakamitanoijayoiweke  jitihadazamakusudikatikasuala la lisheilikuondoatatizo la udumavunautapiamlonchini. 

Aliomba Wizara ya Kilimo na Mifugo kuhakikisha suala la lishe kwa watanzania linaangaliwa kwa undani ili watu wapate lishe nzuri badala ya kuishia kuzungumza bila vitendo na uwepo umoja kwa kila mmoja.

Naye GraceGitauMratibuwaKitaifawamasualayalishenchiniKenyaalielezeamalengoyaliyofikiwakatikauzinduzihuonamipangoyabaadayekuhakikishanchihizozinatengabajetiyalishe 

Gitau alisema kwa Kenya imepiga hatua kwa kuangalia watoto waliodumaa kutokana na ukosefu wa lishe kwa mwaka 2008 na hivyo kupunguza utapia mlo kwa watoto waliochini ya miaka mitano kutoka asilimia 35% hadi 20% kwa sasa.

Alisema moja ya mambo waliyozungumzia ni kutenga kiwago cha fedha ili kukabiliana na tatizo la utapia mlo, katika miradi ya  Afya,kilimo, elimu na maji.

Aliongeza kuwa kupitia miradi hiyona nchi husika zikizingatia kutenga bajeti katika suala la lishe zitaweza kupambana na utapia mlo.

Aidha alisema waluzungumzia suala la kuangali Bajeti za kila mwaka kwa masuala ya lishe iwapo zinakidhi kupambana na utapia mlo.

Kulingana na utafiti ulifanyika mwaka ulipita nchi zote za Afrika Mashariki ni nchi mbili tu ambazo zilifanikiwa kutenga bajeti ya lishe ambayo kwa kiasi fulani ingesaidia.

Alisema kuwa kati ya nchi inazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki ukiangalia utagundua  kwamba Ethiopia walikuwa na asilimia 67%kulingana na lengo la nne ambalo wanapaswa kutimiza kupunguza hali ya lishe.

Burudi ina asilimia 5% ambayo imekuwa chini kati ya malengo waliyojiwekea,Rwanda ni ya pili ambayo imefikisha kiwango kwa kuwa na asilimia 56%,  Kenya asilimia 44% Uganda asilimia 43% Tanzania asilimia 40%  ambapo awali ilikuwa na asilia 42%.Utafiti huo ni kwa miaka miaka mitano iliyopita.

Naye Mkurugenzi wa Jukwaa la Lishe Tanzania (PANITA) alisema hali ya lishe katika ukanda wa Afrika ni mbaya, kwa kuwa ni nchi chache zenye nafuu kupambana na lishe, Tanzania ikiwa ni miongoni mwa nchi hizo.

Alisema ingawa Tanzania ina malengo ya kuondoa tatizo la lishe ifikapo mwaka 2025 juhudi za kutokomeza hali hiyo zinahitajika si tu kwa serikali bali mashirika yasiyo ya kiserikali na watu binafsi.  

Ripoti ya lishe Kimataifa kwa mara ya kwanza ilizinduliwa mwaka 2014 ikiwa na kauli mbiu "Kuulisha Ulimwengu, Kuilea Dunia" ambayo ilichaguliwa kwa lengo la kuongeza hamasa kuimarisha kilimo cha familia na wakulima wadogo wadogo.

Aliongeza kuwa maadhimisho hayo pia yalilenga kuuzindua ulimwengu kuhusu jukumu la kutokomeza njaa na umaskini, kuhakikisha kuna usalama wa upatikanaji wa chakula na lishe bora, kuboresha kipato, kusimamia vyema raslimali, kuyalinda mazingira na kufanikisha maendeleo endelevu, hususan katika maeneo ya mikoani.

Nchizilizoshirikiuzinduzihuonipamoja na Kenya, wenyeji Tanzania, Uganda, Ethiopia,Burudi, Rwanda na Malawi ambaowalishirikikamawasikilizaji. 

 End 

Read more...

Vidonda vya tumbo vyawatesa watanzania

IMEELEZWA kuwa Wafanyakazi na wananchi wengi nchini wamekuwa wakisumbuliwa na ugonjwa wa vidondaVidonda vya tumbo vyawatesa watanzania vya tumbo jambo linalosababisha vifo kutokana na ugonjwa huo.

Sababu kubwa ikiwa ni pamoja na kuwa na msongo wa mawazo kutokana na sababu mbalimbali za kimaisha, kushinda bila kula na kukosekana kwa amani katika jamii.

Hayo yalibainishwa hivi karibuni na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ACP Selemani Kova wakati akipokea Tuzo ya heshima kutoka kwa Rahabu Ulcess Kliniki wakati wa hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya kanda hiyo jijini Dar es Salaam.

Read more...
Tumaini Media

Radio-TV Tumaini, also trading as Tumaini Media, is legally registered in Tanzania under the Business Registration and Licensing Agency (Brela), No 116952. It is a registered Tax payer with TIN 100-251-094 and VRN 10-012753-P. Tumaini Media runs radio and TV stations, and a newspaper namely Radio Tumaini, Tumaini Television and Tumaini Letu, respectively. Tumaini Media seeks to serve the Tanzania community regardless of their colour. race. religion and tribe.

  Jesus is the Patron of our Station

We Now Covering 7 Regions

Coverage has been expanded to include seven out of 21 regions of Tanzania, thus: Tanga, Pwani, Morogoro, Zanzibar, Dar es Salaam and some areas of Dodoma, Kilimanjaro, Iringa and Mbeya Regions.