Menu
RSS
Habari za dunia

Habari za dunia (46)

Waanglikana wamkabidhi zawadi Baba Mtakatifu

ROMA, Italia

UONGOZI na waamini wa Kanisa Anglikana la Watakatifu Wote la Roma nchini Italia, wamemkabidhi Baba Mtakatifu Fransisko zawadi mbalimbali baada ya kufanya ziara ya kihisroria kanisani hapo hivi karibuni.

Miongoni mwa zawadi alizokabidhiwa Baba Mtakatifu ni ahadi ya kutoa chakula kwa ajili ya maskini, Biblia Takatifu kwa ajili ya waathirika wa biashara haramu ya binadamu Barani Afrika na Keki ya Kwaresma.

Jumuiya ya Kanisa hilo iliamua kutoa zawadi hizo kwa ajili ya ziara hiyo ya Baba Mtakatifu ya Februari 26, 2017 iliyoenda sanjari na maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 200 tangu kuanzishwa kwake.

Kwanza waamini wa Kanisa Anglikana la Watakatifu Wote la Roma kwa kushirikiana na Parokia Pacha ya Kanisa Katoliki ya Watakatifu Wote, waliahidi kutoa chakula kila Ijumaa jioni kwa ajili ya maskini wanaorandaranda katika Stesheni ya Treni ya Ostiense, kwa heshima ya Baba Mtakatifu.

Pili, waliahidi kuchapisha nakala 200 za Biblia Takatifu kwa Lugha ya Kiingereza kwa ajili ya jubilei ya Kanisa hilo na kati ya hizo, 50 zitatolewa bure kwa makahaba waliopo nchi za Afrika Magharibi walioomba kupewa msaada huo wa kuwaongoa.

Kwa mujibu wa mpango uliopo, nakala hizo za Biblia Takatifu zitasambazwa kupitia mtandao wa Watawa wanaowasaidia waathirika wa biashara haramu ya biandamu wengi wao wakiishia kushinikizwa kutumiwa katika biashara ya umalaya.

Katika ziara hiyo, Askofu Robert Innes wa Kanisa Anglikana, Jimbo la Ulaya, alimshukuru Baba Mtakatifu Fransisko kwa kutembelea Kanisa la Watakatifu Wote la Roma na kuweka historia ya kuwa Baba Mtakatifu wa kwanza kutembelea Kanisa hilo.

Licha ya Baba Mtakatifu kuwa Askofu wa Roma wa kwanza kufanya ziara kanisani hapo, upo uhusiano mwema kati ya viongozi wakuu wa Makanisa hayo mawili yaani Baba Mtakatifu na Askofu Mkuu wa Canterbury aliye Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana kama alivyo Baba Mtakatifu kwa Kanisa Katoliki.

Tangu Baba Mtakatifu alipochaguliwa kuliongoza Kanisa Katoliki mwaka 2013, Askofu Mkuu wa Canterbury, Justin Welby, ameshakutana mara tatu na kuzungumza na Baba Mtakatifu Fransisko.

Read more...

Vatican kushiriki miaka 60 ya Uhuru wa Ghana

VATICAN CITY, Vatican

RAIS wa Serikali ya Mji wa Vatican, Mwadhama Giuseppe Kardinali Bertello, anatarajiwa kumwakilisha Baba Mtakatifu Fransisko katika maadhimisho ya miaka 40 ya Uhusiano wa Kidiplomasia kati ya Serikali ya Ghana na Vatican.

Idara ya habari ya Vatican ilieleza kuwa maadhimisho hayo yaliyoanza Machi 3 na kufikia kilele chake Machi 6, 2017, yatakwenda sanjari na Kilele cha miaka 60 ya Uhuru wa Ghana.

Ilielezwa katika taarifa hiyo ya Vatican kwamba Ghana iliyojipatia Uhuru wake na kuwekwa wakfu kwa Moyo Mtakatifu wa Yesu, Machi 6, 1957 iko kwenye Novena iliyoanza Februari 23 na kumalizika Ijumaa Machi 3.

Hatua ya Vatican kumtuma Kardinali Bertello kumwakilisha Baba Mtakatifu katika maadhimisho hayo kulielezwa kuwa ni kuonesha Vatican inavyothamini uhusiano uliopo kati ya Kanisa Katoliki na Serikali za mataifa mengine. 

Akieleza kuhusu maadhimisho hayo, mratibu wake kwa upande wa kiroho, Askofu Mkuu Charles G. Palmer-Buckle, alisema Baraza la Maaskofu Katoliki Ghana linataka kuiweka wakfu nchi hiyo chini ya Ulinzi wa Moyo Mtakatifu wa Yesu.

Askofu Palmer-Buckle alibainisha kuwa tendo hilo la kuiweka Wakfu familia ya Mungu nchini Ghana litafanyika wakati wa maadhimisho hayo katika ibada ya Kiekumene itakayoongozwa na Askofu Mkuu Jean-Marie Speich.

Makamu huyo wa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Ghana alisema, Maaskofu waliamua kufikia hatua hiyo kwa kuwa Moyo Mtakatifu wa Yesu ni chemchem ya huruma, neema ya Mungu, msamaha, upendo, unyenyekevu, upole na maisha mapya.

Alisema, Moyo Mtakatifu wa Yesu ni kiini cha Sakramenti za Kanisa uliotobolewa kwa mkuki na kutoka Maji na Damu zilizo alama ya Sakramenti ya Ubatizo na Ekaristi Takatifu.

“Moyo Mtakatifu wa Yesu ni kiini cha Sakramenti za Kanisa uliotobolewa kwa mkuki na kutoka Maji na Damu zilizo alama ya Sakramenti ya Ubatizo na Ekaristi Takatifu” alisema Askofu Palmer-Buckle.

Makamu huyo wa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Ghana alisisitiza kuwa Moyo Mtakatifu wa Yesu ni mwanzo na hatima ya maisha na utume wa Kanisa, chemchemi ya utakatifu na ukamilifu wa maisha ya Kikristo.

Mchakato wa Benedikto XIII kuwa Mtakatifu wafungwa

ROMA, Italia

MAKAMU Askofu wa Jimbo Kuu la Roma, Mwadhama Agostini Kardinali Vallini, ameadhimisha ibada maalumu ya kufunga mchakato wa kutangazwa Mwenyeheri na Mtakatifu, Mtumishi wa Mungu Papa Benedikto XIII.

Kardinali Vallini aliadhimisha ibada hiyo Ijumaa Februari 24, 2017 iliyofanyika katika Jengo la Kitume Laterano na kuwashirikisha wajumbe wa Mahakama ya Jimbo la Roma walioendesha mchakato mzima.

Miongoni mwa wajumbe wa Mahakama hiyo ni Monsinyori Giuseppe D’Alonzo, aliyekuwa Hakimu, mhamasishaji wa amani, Padri Giorgio Cucci na mwandishi wa Hati za Sheria, Marcello Terramani.

Papa Benedikto wa XIII aliyebatizwa kwa jina la Pier Fransisko Orsini, alizaliwa huko Gravina Februari 2, 1649 na Ferdinando III mtu wa cheo katika mji wa Gravina na mama yake alikuwa Giovanna Frangipai aliyezaliwa katika ukoo wa mtu mwenye cheo kikubwa wa Grumo nchini Italia.

Papa Benedikto wa XIII alikuwa mtoto wa kwanza kati ya watoto 6, ingawa alibaki yatima mapema baada ya baba yake kufariki dunia hivyo akachukua nafasi ya baba yake kuwajibika kutunza familia yake hata mama yake.

Licha ya kuwa katika wajibu wa kutunza familia, akiwa bado mdogo alijisikia wito kwa nguvu ndani ya moyo wake, hivyo akaamua kwenda Venezia, Italia alikokamilisha ndoto yake.

Huko Venezia, Pier Fransisko Orsini alipokelewa na Shirika la Wadomenikani, waliokuwa wainjilishaji na kuvaa nguo ya kitawa Agosti 12, 1668 na kubadili jina na kuwa Ndugu Vincenzo Maria.

Alipata Daraja la Upadri Februari 24, 1671 na tarehe 22 Februari 1672 akiwa karibu na miaka 22, Papa Clementi XI akamteua Padri Vincenzo Maria kuwa Kardinali.

Kwa miaka iliyofuatia, Kardinali Vincenzo Maria aliteuliwa kuwa Rais wa Baraza la Kipapa la Maridhiano hadi alipochanguliwa kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Manfredonia, Januari 28, 1675.

Machi 7, 1724 Papa Incocenzo XIII alipofariki dunia, ilichuka muda wa miezi mitatu, kumpata mrithi wake kabla ya Kardinali Vincenzo Maria Orsini kukubali kubadilisha jina lake na akachaguliwa Mei 29, 1724.

Lakini pamoja na hayo ilibidi kwa nguvu zote abadili hilo jina na ndiyo akachangua jina la Papa Benedikto XIII na kitendo cha kuchaguliwa kuwa papa alikifanya abadilishe tabia yake aliyokuwa nayo awali.

Papa Benedikto XIII alifikia hataaua ya kupunguza hata idadi ya walinzi wake waliokuwa wakimsindikiza kila mara alipotoka na kwenda na kundi dogo na aliitisha Mwaka wa Jubilei 1725 ikiwa ni miaka mingi tangu kipindi cha Papa Innocent III.

Papa Benedikto XIII alifariki dunia Februari 21, 1930 akiwa na umri wa miaka 81, akaaga dunia na masalia yake yaliondolewa katika Kanisa la Mtakatifu Maria Sopra Minerva Februari 22, 1733 na kwa sasa yapo katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, Vatican.ROMA, Italia

MAKAMU Askofu wa Jimbo Kuu la Roma, Mwadhama Agostini Kardinali Vallini, ameadhimisha ibada maalumu ya kufunga mchakato wa kutangazwa Mwenyeheri na Mtakatifu, Mtumishi wa Mungu Papa Benedikto XIII.

Kardinali Vallini aliadhimisha ibada hiyo Ijumaa Februari 24, 2017 iliyofanyika katika Jengo la Kitume Laterano na kuwashirikisha wajumbe wa Mahakama ya Jimbo la Roma walioendesha mchakato mzima.

Miongoni mwa wajumbe wa Mahakama hiyo ni Monsinyori Giuseppe D’Alonzo, aliyekuwa Hakimu, mhamasishaji wa amani, Padri Giorgio Cucci na mwandishi wa Hati za Sheria, Marcello Terramani.

Papa Benedikto wa XIII aliyebatizwa kwa jina la Pier Fransisko Orsini, alizaliwa huko Gravina Februari 2, 1649 na Ferdinando III mtu wa cheo katika mji wa Gravina na mama yake alikuwa Giovanna Frangipai aliyezaliwa katika ukoo wa mtu mwenye cheo kikubwa wa Grumo nchini Italia.

Papa Benedikto wa XIII alikuwa mtoto wa kwanza kati ya watoto 6, ingawa alibaki yatima mapema baada ya baba yake kufariki dunia hivyo akachukua nafasi ya baba yake kuwajibika kutunza familia yake hata mama yake.

Licha ya kuwa katika wajibu wa kutunza familia, akiwa bado mdogo alijisikia wito kwa nguvu ndani ya moyo wake, hivyo akaamua kwenda Venezia, Italia alikokamilisha ndoto yake.

Huko Venezia, Pier Fransisko Orsini alipokelewa na Shirika la Wadomenikani, waliokuwa wainjilishaji na kuvaa nguo ya kitawa Agosti 12, 1668 na kubadili jina na kuwa Ndugu Vincenzo Maria.

Alipata Daraja la Upadri Februari 24, 1671 na tarehe 22 Februari 1672 akiwa karibu na miaka 22, Papa Clementi XI akamteua Padri Vincenzo Maria kuwa Kardinali.

Kwa miaka iliyofuatia, Kardinali Vincenzo Maria aliteuliwa kuwa Rais wa Baraza la Kipapa la Maridhiano hadi alipochanguliwa kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Manfredonia, Januari 28, 1675.

Machi 7, 1724 Papa Incocenzo XIII alipofariki dunia, ilichuka muda wa miezi mitatu, kumpata mrithi wake kabla ya Kardinali Vincenzo Maria Orsini kukubali kubadilisha jina lake na akachaguliwa Mei 29, 1724.

Lakini pamoja na hayo ilibidi kwa nguvu zote abadili hilo jina na ndiyo akachangua jina la Papa Benedikto XIII na kitendo cha kuchaguliwa kuwa papa alikifanya abadilishe tabia yake aliyokuwa nayo awali.

Papa Benedikto XIII alifikia hataaua ya kupunguza hata idadi ya walinzi wake waliokuwa wakimsindikiza kila mara alipotoka na kwenda na kundi dogo na aliitisha Mwaka wa Jubilei 1725 ikiwa ni miaka mingi tangu kipindi cha Papa Innocent III.

Papa Benedikto XIII alifariki dunia Februari 21, 1930 akiwa na umri wa miaka 81, akaaga dunia na masalia yake yaliondolewa katika Kanisa la Mtakatifu Maria Sopra Minerva Februari 22, 1733 na kwa sasa yapo katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, Vatican.

Read more...

Walutheri kusherehekea miaka 500 ya mageuzi

LUND, Uswisi

JUBILEI ya miaka 500 ya Mageuzi ya Kiluteri inatarajiwa kuadhimishwa Jumatatu ya Oktoba 31, 2016 huko Lund na Malmo nchini Uswiss.

Maadhimisho hayo yanatarajiwa kufanywa kwa ushirikiano kati ya Kanisa Katoliki na Shirikisho la Makanisa ya Kiinjili ya Kiluteri Duniani.

Kufuatia maadhimisho hayo, Baba Mtakatifu Fransisko anatarajiwa kufanya hija ya kitume nchini Uswis ili kushiriki maadhimisho hayo ya kihistoria katika maisha na utume wa Kanisa.

Licha ya changamoto kadhaa, makanisa hayo mawili yamefaulu kupita hasa ikizingatiwa kuwa, maadhimisho hayo yanafanyika ndani ya kipindi cha miaka 50 tangu Kanisa lianzishe mchakato wa majadiliano ya kiekumene kati ya Kanisa Katoliki na Kanisa la Kilutheri.

Chimbuko la maadhimisho hayo ni Martin Luther ambaye mwaka 1517, alilaani kwa nguvu zake zote vitendo vilivyokuwa vimejitokeza vya kuuza rehema kwa kuzingatia msingi ya maisha ya kiroho na teolojia, hivyo kuleta mageuzi makubwa katika medani za kisiasa, kiuchumi, kiroho na kijamii.

Martin Luther hakuwa na wazo la kuanzisha Kanisa jipya, lakini kutokana na matukio yale, alijikuta analazimika kuanzisha Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Duniani, hivyo kusababisha machafuko na mgogoro ndani ya Kanisa.

Maadhimisho ya kumbukumbu hiyo yaliyofikia miaka 500, kwa muda wa miaka mingi yalikuwa ni sawa na kurasa chungu za misigano kati ya Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Duniani.

Lakini kwa mwaka huu, mambo ni tofauti kabisa, kwani Wakristo wanataka kujikita zaidi katika mambo yanayowaunganisha badala ya kuogelea mambo yanayowagawa.

Kwa sababu hiyo, Baba Mtakatifu Fransisko ameamua kushiriki kikamilifu katika tukio hilo la kihistoria litakalofanyika Lund na Malmo nchini Uswiss.

Lengo ni kuiangalia Jubilei ya miaka 500 ya Mageuzi ya Kilutheri kwa jicho la matumaini pamoja na kuendelea kuimarisha mafanikio yaliyokwisha kupatikana kama sehemu ya mchakato wa majadiliano ya kiekumene katika kipindi cha miaka 50 iliyopita.

Mababa wa Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican walisisitiza kwa namna ya pekee maridhiano kati ya waamini wa Makanisa hayo mawili na kwamba, Sakramenti ya Ubatizo ni kiini cha imani yao kwa Kristo na Kanisa lake na hivyo wote ni sehemu ya Fumbo la Mwili wa Kristo yaaani Kanisa.

Jubilei ya miaka 500 ya Mageuzi ya Kiluteri ni fursa ya kukuza na kuimarisha mahusiano mazuri yaliyofikiwa baina ya Makanisa hayo mawili katika Uekumene wa huduma unaoshuhudiwa na waamini wa Makanisa hayo mawili sehemu mbalimbali duniani.

Katika kipindi cha miaka 10 iliyopita kumekuwepo na mafanikio yaliyofikiwa na kutiwa saini kwenye Waraka wa pamoja kuhusu Mafundisho ya “Kuhesabiwa haki ndani ya Kanisa” yaliyotiwa sahihi kati ya Makanisa haya kunako mwaka 1999.

Dhana ya kuhesabiwa haki ilikuwa ni kiini cha mpasuko kati ya Makanisa hayo katika Karne ya XVI.

Jubilei ya miaka 500 ya Mageuzi ya Kiluteri yanaongozwa na kauli mbiu “Kutoka katika kinzani kuelekea kwenye umoja. Tumeungana katika matumaini”. 

Read more...

Kanisa lataka mshikamano DRC

KINSHASA, DRC

BARAZA la Maaskofu Katoliki Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), limesema makubaliano yaliyofikiwa na vyama vya kisiasa nchini humo kuhusu uchaguzi mkuu, hayana budi kujikita zaidi katika ustawi, maendeleo na maslahi ya wananchi wengi.

Kwa mujibu wa Mtandao wa Vatican, Maaskofu hao walitoa tamko lao na kutaka makubaliano hayo yasiangalie faida zinazoweza kupatikana kwa vyama vya siasa husika pekee na viongozi wake.

Maaskofu hao walikubaliana kimsingi katika tamko hilo kwamba, wakati wa kipindi cha mpito kutaundwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa itakayokuwa kweli na sura ya kitaaifa.

Mapendekezo yao ni kuona Serikali hiyo inakuwa na Waziri Mkuu atakayetoka vyama vya upinzani wakati Rais Joseph Kabila anayemaliza muda wake, akiendelea kuwa kiongoza wa DRC.

Kabla ya kutoa tamko hilo wakati wajumbe kutoka Baraza la Maaskofu Katoliki DRC walijitoa katika majadiliano kati ya Serikali na vyama vya upinzani, kwa sababu ya kukosekana kwa uwakilishi mpana wa vyama vyote vya upinzani.

Maaskofu hao walisema, mmbo ya msingi yanayotakiwa kupewa kipaumbele ni maandalizi ya uchaguzi mkuu, haki za msingi za binadamu, kuyafanya maisha ya wananchi kuwa bora zaidi kwa njia ya huduma za jamii hasa afya, elimu na uchumi.

Katika tamko lao, Maaskofu walieleza kuwa Baraza la Maaskofu Katoliki DRC linataka kujielekeza zaidi katika kukuza na kudumisha misingi ya haki, amani, maridhiano, umoja na mshikamano wa kitaifa.

Read more...

Makazi ya Papa ya Castel Gandolfo kuwa makumbusho

VATICAN CITY, Vatican

IKULU Ndogo ya Castel Gandolfo iliyoko nje kidogo ya Mji wa Roma nchini Vatican, inayotumiwa na Baba Mtakatifu wakati wa majira ya joto, sasa imekuwa moja ya Makumbusho ya Vatican. 

Kwa mara ya kwanza katika historia ya Kanisa, Ikulu hiyo ndogo ya Vatican imefunguliwa rasmi kuwa makumbusho kuanzia Jumamosi Oktoba 22, 2016.

Kuanzia siku hiyo yaani Oktoba 22, 2016, mahujaji na wageni mbalimbali wanaofika jijini Roma, wameanza kutembelea Makumbusho ya Castel Gandolfo kama moja ya makumbusho ya Vatican.

Kwa muda wa miaka miwili, Bustani yenye umaarufu wa pekee ya Castel Gandolfo zilikuwa zinatembelewa na wageni kutoka sehemu mbali mbali za dunia.

Baada ya makumbusho hayo kuanza kwa mahujaji kuanza kuyatembelea, hatua inayofuata kwa sasa ni kufungua vyumba vilivyokuwa vinatumiwa na Mapapa katika Ikulu hiyo ndogo wakati wa mapumziko yao.

Kwa wale wanaotumia mitandao ya ajamii, wanaweza kupanga siku maalum ya kutembelea kwa kutumia mtandao kwa anuani ya  www.museivaticani.va

Read more...

Padri Arturo Mkuu mpya Shirika la Wajesuiti

ROMA, Italia

SHIRIKA la Wajesuiti limemchagua Padri Arturo Sosa Abascal kutoka Venezuela, kuwa Mkuu wa Shirika mpya wa shirika hilo lenye makao yake Makao Makuu mjini Roma.

Padri Arturo Sosa alichaguliwa katika Mkutano Mkuu wa 36 wa shirika hilo akichukua nafasi ya Mkuu wa Shirika aliyestaafu, Padri Adolfo Nicolàs aliyeng’atuka Oktoba 3, mwaka huu kutokana na umri mkubwa.

Padri Arturo Sosa aliyezaliwa mwaka 1948, alijiunga na Shirika la Wajesuiti mwaka 1966 na kupewa Daraja Takatifu la Upadri mwaka 1977, anakuwa Mkuu wa Shirika wa 31.

Kabla ya kuchaguliwa na wajumbe wa Mkutano Mkuu uliofanyika mjini Roma, Padri Arturo Sosa alikuwa mwalikishi wa Wakuu wa Kanda wa Shirika la Wajesuiti mjini Roma.

Kati ya mwaka 1996 na mwaka 2004 alikuwa ni Mkuu wa Shirika la Wajesuiti, Kanda ya Venezuela na aliwahi pia kuwa Mratibu wa Shughuli za Kijamii na Mkuu wa Kituo cha Utafiti cha Wajesuiti, Amerika Kusini huko Gumila.

Kwa muda mrefu, Padri Arturo Sosa alitekeleza utume wake kwa kuwalea na kuwafundisha vijana katika masuala ya elimu, kwani kimsingi yeye ni mtaalamu aliyebobea katika masuala ya elimu na ni mwandishi mahiri wa vitabu hasa kuhusu historia na siasa ya maisha ya familia ya Mungu nchini Venezuela.

Padri Adolfo Nicolàs akiwa Mkuu wa Shirika, mwaka 2008 katika Mkutano Mkuu wa 35, Arturo Sosa aliteuliwa kuwa Mshauri Mkuu na mwaka 2014 akateuliwa kuwa mmoja wa washauri wakuu wa shirika hilo.

Katika mkutano Mkuu wa shirika wa Roma mwaka huu, wajumbe 212 kutoka nchi 66 walishiriki.

MASAHIHISHO

Katika toleo lililopita tulichapisha habari ya Shirika la Wajesuiti kupata Mkuu wa Shirika mpya. Hata hivyo katika habari hiyo kulikuwa na makosa kadhaa ikiwemo kuliita Shirika la Majeswiti badala ya Wajesuiti na kueleza kuwa Mkuu wa Shirika aliyetangulia, Padri Adolfo aling’atuka badala ya kustaafu. Kutokana na upungufu huo, tumeirudia habari hiyo kwa usahihi Tunaomba radhi kwa usumbufu na tunamshukuru Padri Zachary Miricho SJ, wa Loyola High School, Dar es Salaam, kwa masahihisho.

Read more...

Baba Mtakatifu awakumbuka waathirika wa Kimbunga Matthew

POT-AU-PRINCE, Haiti

BABA Mtakatifu Fransisko ameungana na watu wote walioguswa na kutikiswa kwa Kimbunga Matthew kilichovikumba Visiwa vya Carribean, lakini kwa namna ya pekee, Haiti.

Baba Mtakatifu alionesha masikitiko yake hayo wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana, baada ya maadhimisho ya Jubilei ya Bikira Maria, maalum kwa vyama vya kitume vyenye ibada kwa Bikira Maria Mama wa Mungu na Kanisa iliyofanyika Dominika ya 28 ya Mwaka C wa Kanisa.

Akihutubia mahujaji waliofika kwenye Viwanja vya Mtakatifu Petro, Vatican, Baba Mtakatifu aliwaambia mahujaji hao kwamba alikuwa ameguswa kwa namna ya pekee na maafa makubwa yaliyotokana na kimbunga hicho.

Alisema, angependa kuonesha uwepo wake wa karibu na matumaini makubwa kwa mshikamano unaoendelea kuoneshwa na jumuiya ya kimataifa, taasisi za Kanisa pamoja na watu wote wenye mapenzi mema.

Baba Mtakatifu alisema, anawaalika waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kuungana naye katika sala kwa ajili ya watu hao walioathirika kwa kiasi kikubwa.

Haiti ilipata athari kubwa kutokana na Kimbunga Matthew kilichoua watu wapatao mia tisa, kuharibu maelfu ya nyumba na kusababisha watu 350,000 kuwa katika hali ya kuhitaji misaada.

Hata hivyo, Serikali ya Haiti ilieleza kuwa idadi rasmi ya watu waliofariki dunia na kuthibitishwa ni 336, ingawa idadi inaweza kuwa kubwa zaidi kwa kuwa wengi katika maeneo ya vijijini hawakuweza kufikiwa kwa sababu ya kukatika kwa barabara na kuvunjika kwa madaraja.

Katika sala hiyo ya Malaika wa Bwana, Baba Mtakatifu alimkumbuka Padri Gennaro Fueyo Castanon na waamini walei watatu waliotangazwa kuwa Wenyeheri huko Oviedo, Hispania, Jumamosi Oktoba 8, 2016.

Baba Mtakatifu alimshukuru Mungu Mwenyezi kwa mashuhuda hao wa imani wanaoungana sasa na umati mkubwa Mashahidi wa Imani walioyamimina maisha yao kwa ajili ya Kristo na Kanisa lake.

Read more...

Kanisa lataka amani Ghana kuelekea uchaguzi

TAMALE, Ghana

BARAZA la Maaskofu Katoliki Ghana (GCBC) limetoa wito kwa waamini na wananchi wote wa nchi hiyo kudumisha amani wakati nchi hiyo ikijiandaa kwa Uchaguzi Mkuu utakaofanyika baadaye Desemba 7 mwaka huu.

Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Ghana na Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Konongo-Mampong, Mhashamu Joseph Osei-Bonsu, alitoa wito huo kupitia Mkutano Mkuu wa GCBC uliofanyika hivi karibuni katika mji wa Kaskazini wa Tamale.

Askofu Osei-Bonsu alisema, Ghana imekuwa katika wakati mzuri wa amani na utulivu iliyopo hadi sasa aliyosema inatakiwa kulindwa na kila mwananchi wa Ghana mwenye mapenzi mema.

Alisema, wananchi wote wa Ghana wanatakiwa kukumbuka kuwa wana nchi moja tu nayo ni Ghana nayo ndiyo nyumba ya kila mwananchi wa Ghana inayotakiwa kulindwa kwani ndimo wanamoishi.

“Wananchi wote wa Ghana tunatakiwa kukumbuka kuwa tuna nchi moja tu nayo ni Ghana nayo ndiyo nyumba ya kila mwananchi wa Ghana inayotakiwa kulindwa kwani ndimo tunamoishi” alisema, Askofu  Osei-Bonsu.

Osei-Bonsu alaisema, wananchi wa Ghana wasingetaka kuoma machafuko yakitokea kabla, wakati au baada ya uchaguzi kwani wamezoea kuishi kwa amani na upendo.

Aliwakumbusha wananchi wa Ghana kwamba matokeo ya machafuko yanajulikana kwa kila mtu ikiwemo kupotea kwa maisha ya binadamu, majeruhi na uharibifu wa mali, hofu na hatimaye kuibuka kwa wimbi la wakimbizi.

Askofu Osei-Bonsu alisema, wananchi wa Ghana hawataki kuwa wakimbizi katika nchi jirani kwa sababu ya machafuko yatakayotokana na uchaguzi.

“Wananchi wa Ghana hawataki kuwa wakimbizi katika nchi jirani kwa sababu ya machafuko yatakayotokana na uchaguzi” alisisitiza Askofu Osei-Bonsu.

Maaskofu 20 wa Baraza la Maaskofu Katoliki Ghana wameshiriki Mkutano Mkuu huo wa siku 10 wa GCBC ulioongozwa na kauli mbiu ‘Upatanisho na Mungu, Utu na Asili katika Mwaka wa Huruma ya Mungu’

Read more...
Subscribe to this RSS feed
Tumaini Media

Radio-TV Tumaini, also trading as Tumaini Media, is legally registered in Tanzania under the Business Registration and Licensing Agency (Brela), No 116952. It is a registered Tax payer with TIN 100-251-094 and VRN 10-012753-P. Tumaini Media runs radio and TV stations, and a newspaper namely Radio Tumaini, Tumaini Television and Tumaini Letu, respectively. Tumaini Media seeks to serve the Tanzania community regardless of their colour. race. religion and tribe.

  Jesus is the Patron of our Station

We Now Covering 7 Regions

Coverage has been expanded to include seven out of 21 regions of Tanzania, thus: Tanga, Pwani, Morogoro, Zanzibar, Dar es Salaam and some areas of Dodoma, Kilimanjaro, Iringa and Mbeya Regions.