Menu
RSS
Tanzania

Tanzania na Brazil,zaingia makubaliano kilimo cha Pamba

MWANZA

Tanzania na Brazil zimeingia makubaliano ya kuinua kilimo cha zao la pamba ili kiwe na tija kwa wakulima nchini, wakati Brazil ikiwa katika hatua kubwa za kimageuzi ya kilimo.

Naibu Waziri wa Kilimo, INNOCENT BASHUNGWA ameyasema hayo, baada ya kutembelea na kukagua mashamba ya mfano wa kilimo cha pamba, katika Kituo cha Utafiti-TARI, Ukiriguru mkoani Mwanza.

Naibu Waziri BASHUNGWA amesema kuwa, mradi wa kuinua kilimo cha pamba unaotekelezwa na Brazil katika katika nchi tatu za Burundi, Kenya na Tanzania, utajielekeza zaidi katika kuwahakikishia wakulima, pamba mbegu bora.

 Amesema kuwa, kupitia mradi huo, uzinduzi wa utafiti wowote utakaofanywa kwa ajili ya mageuzi ya kilimo cha pamba nchini, ni lazima utamfikia mkulima ili aweze kuongeza tija.

Naibu Waziri BASHUNGWA amesisitiza kuwa, Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Rais Dakta JOHN POMBE MAGUFULI, imedhamiria kwa kauli moja, kuimarisha sekta ya kilimo, likiwemo zao la pamba.

 

Na. Martin Kuhanga

Read more...

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam,Kuomba zabuni mabasi yaendayo haraka

DAR ES SALAAM

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam linakusudia kuomba zabuni ya kutoa huduma ya kusafirisha abiria kupitia mabasi yaendayo haraka kati ya Gerezani, Kariakoo na Mbagala.  Mstahiki Meya wa Jiji, ISAYA MWITA, amebainisha hayo baada ya kumalizika kwa kikao cha Baraza la Madiwani, kilichofanyika leo, katika Ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam.

 Meya Mwita amesema kuwa tayari Wakala wa mabasi yaendayo haraka wameshatangaza zabuni ya ujenzi wa awamu ya pili ya miundombinu ya mabasi itakayoanzia Kegerezani hadi Mbagala hivyo kama jiji limeona kunahaja ya kuomba zabuni hiyo ilikutoa huduma hiyo ya usafiri.

Amefafanua kuwa jiji linania ya kuomba zabuni hiyo kutokana na kuwa wanaweza kutoa huduma hiyo ili kusaidia adha ya foleni iliyopo kwa sasa katika maeneo ya Mbagala.

“ Tunatarajia kuomba zabuni ya kutoa huduma ya kusafirisha abiria hapa jijini ,iwapo tutakubaliwa basi kama jiji nalo litakuwa miongoni mwa watoa huduma hiyo” amesema Meya Mwita.

Tunajua kwamba pesa tunazo, nauwezo wakutoa huduma hiyo tunao,kwahiyo wakazi wa jijini hapa wafahamu kuwa kama tutakubaliwa tutatoa huduma hiyo, ndio mana leo nimewaeleza madiwani kwamba uliangalie jambo hili kwa umuhimu wake ilitujiandae” ameongeza.

Katika hatua nyingine baraza hilo limepitisha kwa kauli moja taarifa mbalimbali za utendaji na miradi mbalimbali zilizotolewa na wenyeviti wa kamati  mbalimbalimbali za jiji.

Mwishoo.

Imetolewa leo Machi 12 na Christina Mwagala .Afisa habari ofisi ya meya wa jiji.

***

 

Frida Manga

Read more...

SHIRIKISHO LA KWAYA KATOLIKI DAR ES SALAAM KUFANYA TAMASHA

DAR ES SALAAM

Shirikisho la kwaya Jimbo Kuu katoliki la Dar es Salaam,Dominika hii linatarajiwa kufanya tamasha la kwaya kwaajili ya uinjilishaji ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka hamsini ya Ukristo Tanzania Bara.

Tamasha hilo linatarajiwa kuanza majira ya saa sita kamili mchana 6.00 katika viwanja vya msimbazi Center na kuhuduriwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, mwadhama KARDINAL PENGO .

Tamasha hilo linatarajiwa kushirikisha kwaya kutoka dekania zote tisa za Jimbo Kuu la Dar es salaam.

Pamoja na shirikisho la kwaya Katoliki kutoka parokia ya Msimbazi taarifa iliyotolewa na SIXBERT MGAHUZI amesema mwenyekiti wa shirikisho.

Amesema tamasha hilo lina lengo kuenzi na kuutangaza mwaka wa jubilei ya miaka 150 ya Ukristo Tanzania bara ambao unatarajiwa kuhitimishwa Novemba 4 mwaka katika mlango wa imani Bagamoyo Jimbo Katoliki la Morogoro.

Ashura Kishimba.

 

Read more...

Tanzania yawa na fanikio katika kuokoa vifo vya watoto

DAR ES SALAAM

Wakati maadhimisho ya Siku ya Mtoto Duniani yakifanyika Novemba 20,2017 imeelezwa kuwa, katika miaka ya hivi karibuni, Tanzania imepata mafanikio makubwa katika ulinzi, makuzi na maendeleo ya mtoto.

Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto-UNICEF, nchini Tanzania, MANIZA ZAMAN, amesema, mafanikio hayo ni pamoja na kupungua kwa kiasi kikubwa kwa vifo vya watoto, wenye umri chini ya miaka mitano {5}.  

MANIZA ametaja mafanikio mengine kwa Tanzania ambayo asilimia hamsini {50% ya watu wake wana umri wa chini ya miaka 18, ni kuongezeka kwa huduma ya chanjo kufikia asilimia 75 na kupungua udumavu kwa asilimia thelathini na nne {34%}.

Licha ya mafanikio hayo yote, MANIZA amesema, zipo changamoto pia ikiwemo uwiano usio sawa wa maendeleo hayo kati ya watoto wanaoishi maeneo ya mijini na vijijini.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na UNICEF, watoto zaidi ya milioni mia moja themanini {180 m.}, katika nchi thelathini na saba {37} duniani, wako katika hatari ya kuishi katika umaskini uliokithiri, kukosa masomo na kuuawa kikatili, ikilinganishwa na miaka 20 iliyopita.

Nchi hizo thelathini na saba {37} ni pamoja Benin, Bolivia, Cameroon, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Comoro, Côte d'Ivoire, Djibouti, Equatorial Guinea, Eritrea, Guatemala, Guyana, Guinea-Bissau, Jordan, Iraq, Kiribati, Lebanon, Liberia, Libya, Madagascar, Mali, Visiwa vya Marshall, Micronesia, Palau, Paraguay, Jamhuri ya Moldova, Romania, Saint Kitts and Nevis, Visiwa vya Solomon, Sudan Kusini, Syria, Tonga, Tanzania, Ukraine, Vanuatu. Yemen, Zambia na Zimbabwe.  

***

Martin Kuhanga {Tamko WAMJJWW}

Read more...

Tanzania yawa na fanikio katika kuokoa vifo vya watoto

DAR ES SALAAM

Wakati maadhimisho ya Siku ya Mtoto Duniani yakifanyika Novemba 20,2017 imeelezwa kuwa, katika miaka ya hivi karibuni, Tanzania imepata mafanikio makubwa katika ulinzi, makuzi na maendeleo ya mtoto.

Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto-UNICEF, nchini Tanzania, MANIZA ZAMAN, amesema, mafanikio hayo ni pamoja na kupungua kwa kiasi kikubwa kwa vifo vya watoto, wenye umri chini ya miaka mitano {5}.  

MANIZA ametaja mafanikio mengine kwa Tanzania ambayo asilimia hamsini {50% ya watu wake wana umri wa chini ya miaka 18, ni kuongezeka kwa huduma ya chanjo kufikia asilimia 75 na kupungua udumavu kwa asilimia thelathini na nne {34%}.

Licha ya mafanikio hayo yote, MANIZA amesema, zipo changamoto pia ikiwemo uwiano usio sawa wa maendeleo hayo kati ya watoto wanaoishi maeneo ya mijini na vijijini.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na UNICEF, watoto zaidi ya milioni mia moja themanini {180 m.}, katika nchi thelathini na saba {37} duniani, wako katika hatari ya kuishi katika umaskini uliokithiri, kukosa masomo na kuuawa kikatili, ikilinganishwa na miaka 20 iliyopita.

Nchi hizo thelathini na saba {37} ni pamoja Benin, Bolivia, Cameroon, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Comoro, Côte d'Ivoire, Djibouti, Equatorial Guinea, Eritrea, Guatemala, Guyana, Guinea-Bissau, Jordan, Iraq, Kiribati, Lebanon, Liberia, Libya, Madagascar, Mali, Visiwa vya Marshall, Micronesia, Palau, Paraguay, Jamhuri ya Moldova, Romania, Saint Kitts and Nevis, Visiwa vya Solomon, Sudan Kusini, Syria, Tonga, Tanzania, Ukraine, Vanuatu. Yemen, Zambia na Zimbabwe.  

***

Martin Kuhanga {Tamko WAMJJWW}

Read more...

Uzo la mara moja la TBL kwa Submiller la sababisha kupungua kwa soko la hisa Dar es salaam DSE Tanzania

DAR ES SALAAM

Imeelezwa kuwa uzo la mara moja la hisa za Kampuni ya TBL kwa kampuni tanzu ya SABMiller, limesababisha thamani ya mauzo ya hisa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam-DSE kupungua.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Afisa Mwandamizi Masoko wa DSE, MARY KINABO, amesema, uzo hilo limepungua kutoka Shilingi Billioni 86 ya wiki iliyopita hadi Shilingi Bilioni 1 kwa wiki iliyoishia Ijumaa, Novemba 17.

KINABO amesema, juma lililopita thamani ya mauzo hayo ilipanda kwa kiwango kikubwa kutokana na mauzo hayo ya hisa za TBL kwenda SABLiller.

Aidha, KINABO, amesema, vile vile idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa zimepungua kutoka hisa milioni 9 ya wiki iliyopita hadi hisa milioni tano, nukta tano {5.5m} ya wiki iliyoishia Ijumaa, Novemba 17.

KINABO amesema, ukubwa wa mtaji wa kampuni zote zilizoorodheshwa katika soko umepungua kwa Shilingi Bilioni 412 kutoka Shilingi Trilioni ishirini, nukta nane {20.8t} wiki iliyopita hadi Shilingi Trilioni ishirini, nukta tatu {20.3} wiki iliyoishia iliyoishia Ijumaa, Novemba 17. 

Amesema, punguzo hilo limetokana na kushuka kwa bei za hisa za KA kwa 8%, DSE kwa 7%, KCB kwa 6%, CRDB kwa 6%, NMG kwa 5% na EABL kwa 4%.

KINABO amesema, ukubwa wa mtaji wa kampuni za ndani umeshuka kwa Shilingi Bilioni 28 kutoka shilingi Trilioni kumi, nukta sifuri nane {10.08%} hadi kafika Shilingi Trilioni kumi, nukta sifuri, tano {10.05%}, iliyoishia Ijumaa, Novemba 17, kutokana na kushuka kwa bei ya hisa ya DSE kwa 7%) na CRDB kwa 6%.

Kuhusu mauzo ya hati fungani katika wiki iliyoishia Novemba 17 2017, KIBABO amesema, yalikuwa Shilingi Bilioni tatu, nukta moja, nne {3.14bil} kutoka Shilingi Bilioni kumi na moja, nukta mbili {11.2} wiki iliyopita.

 

Editha Mayemba & Brian Rama-DSJ

Read more...

Jubilee miaka 50 karismatic katoliki kuadhimishwa Pentekoste Roma

ROMA

Kilele cha maadhimisho ya Jubilei ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Karismatiki Katoliki Duniani kinatarajiwa kufanyika katika Sikukuu ya Pentekoste Dominika hii, katika Jimbo Kuu Katoliki la Roma.

Mtandao wa Vatican umeeleza kuwa adhimisho hilo litatanguliwa na mkesha wa Pentekoste siku ya Jumamosi utakaohudhuriwa na Baba Mtakatifu FRANSISKO, kwenye Uwanja wa Circo Massimo Mjini Roma.

Taarifa hiyo imebainisha kuwa Baba Mtakatifu anatarajia kuadhimisha kilele hicho na Dominika ya Pentekekoste kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu PETRO, Vatican kuanzia saa 4:30 kwa saa za Ulaya.

Chama hicho cha Kitume nchini Italia pia kinaadhimisha kumbukumbu ya miaka 40 tangu kuanzishwa kwake jambo ambalo limepewa uzito na makao makuu ya Vatican.

Kwa kutambua uzito wa tukio hilo katika maisha na utume wa Kanisa, Katibu mkuu wa Vatican Mwadhama PIETRO Kardinali PAROLIN, amemtumia ujumbe wa heri na baraka Rais wa Karismatiki Italia Daktari SALVATORE MARTINEZ.

Maadhimisho ya Jubiliei ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Chama hicho ni wakati wa kumshukuru Roho Mtakatifu kwa neema nyingi alizolijalia Kanisa na fursa ya kusikiliza shuhuda za wanachama na changamoto walizokabalina nazo kwa kipindi hicho cha Jubilei ya dhahabu.

Utume wa Karismatiki Katoliki ni matunda ya Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican na tayari wajumbe kutoka ndani na nje ya Italia wameanza kuwasili tayari kushiriki katika semina, makongamano na sala katika makanisa mbali mbali hapa Roma.

***

 

Gaudence Hyera

Read more...

Waleeni watoto katika njia impendezayo Mungu.


 

MOROGORO

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzani(KKKT) Dayosisi ya Morogoro JACOB OLE MAMEO amewataka wazazi na walezi kuwalea watoto kwa kuzingatia misingi ya maadili mema.

Ametoa rai hiyo kwenye maadhimisho ya miaka miwili ya kuwa jimbo kamili ya Kanisa la Moravian Tanzania na kuwahimiza wazazi na walei kutekeleza wajibu wao ili kujenga taifa la watu waadilifu na waaminifu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauru Kuu ya Kanisa hilo Mchungaji SAMWELI MWAISEJE amewatahadharisha Madereva wa vyombo vya moto kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani.

Amekumbusha na kutoa angalizo hilo ili Madereva waweze kukabiliana na matukio ya ajali yanayoendelea kujitokeza na kupoteza maisha ya watu hasa katika kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha.

Mchungaji MWAISEJE amesema Kanisa limesikitishwa na tukio la ajali iliyotokea wilayani Karatu mkoani Arusha na kusababisha vifo vya  wanafunzi 33 wa shule ya Lucky Vincent, walimu 2 na dereva wao.

Ameongeza kuwa matukio hayo ya ajali yanawezesha kudhibitiwa iwapo watumiaji wa vyombo hivyo watazingatia sheria za usalama barabarani.

Aidha Mchungaji MWAISEJE ameipongeza Serikali kwa jitihada za kuendelea kudhibiti mianya ya udanganyifu wa vyeti yaani vyeti feki kwa watumishi wa umma.

***

Merina Robert

Read more...

Mahujaji 36 wakatoliki Tanzania waondoka ureno kushiriki miaka 100 ya Bikira Maria wa Fatima

DAR ES SALAAM.

        Mahujaji thelathini na Sita kutoka Jimbo kuu Katoliki la Dar es Salaam waondoka  leo Mey 9,2016 kwenda Fatima nchini Ureno kwa ajili ya kushiriki Jubilei ya Miaka Moja ya Tokeo la Bikira MARIA.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Uchungaji Jimboni humo Padri-Daktari JOSEPH MATUMAINI, Safari hiyo inatarajiwa kuanzia Usiku wa kuamkia Jumatano.

Amesema Mahujaji wote leo wamefanya Tafakari ya mafungo yaliyoongozwa na Katibu wa Jimbo hilo Padri AIDAN MUBEZI katika Ukumbi wa Kanisa kuu la Mtakatifu YOSEFU,Jimboni humo.

Padri MATUMAINI amebainisha kuwa miongoni mwa Mahujaji hao wamo Mapadri wanne, Watawa watatu na Waamini Walei Ishirini na tisa ambao watasafiri kwa pamoja.

Ameongeza kuwa wakiwa Ureno watatembelea Madhabahu ambayo Mama Bikira Maria aliwatokea watoto wa Familia moja Mwenyeheri Sista LUSIA na Watakatifu watarajiwa FRANSISKO na YASINTA.

Padri MATUMAINI ambaye pia ni Paroko wa Kanisa Kuu la Mtakatifu YOSEFU amesema Jumamosi hii mahujaji hao watashiriki adhimisho la kilele cha hija hiyo pamoja na Baba Mtakatifu FRANSISCO.

Mahujaji hao wote wanatarajia kuanza safari ya kurejea nyumbani Jumanne ijayo Mei 16.

***

Gaudence Hyera

 

Read more...

Askofu apigwa na butwaa waamini kuendelea na shughuli zao Dominika

DAR ES SALAAM

Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar Es Salaam Mhashamu EUSEBIUS NZIGILWA amewashangaa waamini wanaoacha Kusali Ibada ya Dominika na kwenda kwenye shughuli nyingine za Kijamii.

Ameonyesha mshangao huo alipokuwa akitoa Mahubiri yake kwenye adhimisho la Misa Takatifu Dominika ya jana iliyofanyika katika Parokia ya Bikira MARIA wa Mateso Msakuzi, Jimboni humo.

Askofu NZIGILWA amewahimiza waamini kumtafuta Mungu badala ya kukimbilia kutafuta mahitaji mengine ya kidunia ambayo yeye anao uweza wa kuwapatia maradufu ikiwa watamtumainia kwa imani.

Katika adhimisho hilo ambalo Askofu NZIGILWA ametoa Sakramenti ya Kipaimara kwa vijana sabini na nane wa Parokia hiyo, amewataka waamini kutambua kuwa wakimkosa KRISTO wajue wamekosa yote.

Amewahimiza vijana waimarishwa kuwa watu wa Sala na kumtegemea KRISTO Mchungaji mwema na kumuomba awe mlinzi katika nyumba wanamoishi kinyume chake watakuwa kama wanaishi Maporini.

Sanjari na adhimisho hilo pia Askofu NZIGILWA amebariki na kuizindua nyumba mpya ya Mapadri iliyojengwa kwa nguvu ya michango ya hali na mali ya waamini wa Parokia hiyo.

Amewapongeza Waamini wote kwa ujumla kwa kufanikisha ujenzi wa nyumba hiyo kwa ajili ya wachungaji wao iliyogharimu zaidi ya shilingi Milioni Mia Tatu Arobaini.

Askofu NZIGILWA aliongoza Harambee ya kuchangia Ujenzi wa Kanisa ambapo zaidi ya shilingi Milioni 13 ikiwa ni ahadi pamoja na Fedha Taslimu zilipatikana.

Kwa upande wake Mkuu wa Shirika la Wamisionari Warosmini Afrika Mashariki Padri ENHART MPETE ameahidi kuongeza idadi ya Mapadri wanaofanyakazi Parokiani hapo ili kuimarisha Uinjilishaji.

***

Editha Mayemba/Gaudence Hyera

Read more...
Tumaini Media

Radio-TV Tumaini, also trading as Tumaini Media, is legally registered in Tanzania under the Business Registration and Licensing Agency (Brela), No 116952. It is a registered Tax payer with TIN 100-251-094 and VRN 10-012753-P. Tumaini Media runs radio and TV stations, and a newspaper namely Radio Tumaini, Tumaini Television and Tumaini Letu, respectively. Tumaini Media seeks to serve the Tanzania community regardless of their colour. race. religion and tribe.

  Jesus is the Patron of our Station

We Now Covering 7 Regions

Coverage has been expanded to include seven out of 21 regions of Tanzania, thus: Tanga, Pwani, Morogoro, Zanzibar, Dar es Salaam and some areas of Dodoma, Kilimanjaro, Iringa and Mbeya Regions.