Menu
RSS

TCRA kuhakikisha matangazo kwa Digital Tanzania nzima

TCRA kuhakikisha matangazo kwa Digital Tanzania nzima

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA imesema kuwa itahakikisha kuwa kabla ya mwisho wa uzimaji wa mitambo kimataifa, miji yote nchini iliyokuwa na matangazo ya analogia inapata matangazo ya digitali.

Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja Uhusiano wa Mamlaka hiyo INNOCENT MUNGY amesema kuwa ifikapo Juni kumi na saba mwaka huu, miji ambayo bado ilikuwa ikitumia mitambo ya analogia kuangalia televisheni itakuwa imeingia kwenye mitambo ya digitali.

MUNGY amesema kuwa mpango wa kupeleka teknolojia ya digitali maeneo ya vijijini umependekezwa kuwa na teknolojia ya DHT inayotumia vin’gamuzi vya Setelaiti vikisaidiana na teknolojia ya Terrestrail itakayorahisisha kufikisha teknolojia hiyo vijijini.

Amebainisha kuwa tayari kampuni mbalimbali zimeanza kutoa huduma za utangazaji wa televisheni kwa kutumia teknolojia ya Setelaiti DTH.

Hata hivyo MUNGY amekiri kuwa uwezekano wa kufikisha huduma hizo kwa Tanzania nzima ni mgumu kutokana na ukubwa wa nchi na jinsi makazi ya wananchi wa vijijini yalivyo.

                                                       ***

Ashura Kishimba
DAR ES

Last modified onThursday, 02 April 2015 15:14
More in this category: « WhatsApp yawabana watumiaji
back to top
Tumaini Media

Radio-TV Tumaini, also trading as Tumaini Media, is legally registered in Tanzania under the Business Registration and Licensing Agency (Brela), No 116952. It is a registered Tax payer with TIN 100-251-094 and VRN 10-012753-P. Tumaini Media runs radio and TV stations, and a newspaper namely Radio Tumaini, Tumaini Television and Tumaini Letu, respectively. Tumaini Media seeks to serve the Tanzania community regardless of their colour. race. religion and tribe.

  Jesus is the Patron of our Station

We Now Covering 7 Regions

Coverage has been expanded to include seven out of 21 regions of Tanzania, thus: Tanga, Pwani, Morogoro, Zanzibar, Dar es Salaam and some areas of Dodoma, Kilimanjaro, Iringa and Mbeya Regions.