Tumaini Letu paper
Padri Makuri ahimiza miito
Na Lilian Lihame,Singida
WAAMINI wa Jimbo Katoliki la Singida wametakiwa kutimiza wajibu wao wa kuwalea watoto katika maadili ya Kanisa ili kukuza miito mingi ya upadri na kulisaidia Kanisa.
Wito huo ulitolewa hivi karibuni na Padri Deogratius Makuri alipokuwa akizungumza na Tumaini Letu Jimboni humo.
Jimbo la Singida kwa sasa lina idadi ndogo ya Mapadri na kufanya kazi za uinjilishaji kuwa ngumu hasa kuanzishwa kwa Parokia mpya.
Alisema kuwa wazazi wengi wamekuwa wakikimbia majukumu ya kuwalea watoto na hivyo watoto kujilea wenyewe kitendo kinachosababisha watoto kujifunza mambo mengi kwa wengine badala ya wazazi na walezi wao.
Read more..
Mataifa Afrika yahadharishwa tofauti za kipato
Na Frida Manga
MATAIFA ya Bara la Afrika zimetakiwa kuweka mikakati ya kuondoa tofauti ya watu walionancho na wasionacho, kwani pengo hilo likizidi linaweza kuleta hatari kwa jamii.
Mwenyekiti wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Dk.Edmund Mndolwa alisema hayo hivi karibuni jijini Dar es Salaam wakati akitoa mada kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya Umoja wa Nchi za Afrika (AU).
Alisema kuwa kwa kipindi cha miaka 50 ya sasa katika nchi za Afrika hakuna uwiano kati ya walionancho na wasionacho na kwamba watu walionancho ni wachache ikilinganishwa na wasionacho.
Read more..
Mataifa Afrika yahadharishwa tofauti za kipato
Na Frida Manga
MATAIFA ya Bara la Afrika zimetakiwa kuweka mikakati ya kuondoa tofauti ya watu walionancho na wasionacho, kwani pengo hilo likizidi linaweza kuleta hatari kwa jamii.
Mwenyekiti wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Dk.Edmund Mndolwa alisema hayo hivi karibuni jijini Dar es Salaam wakati akitoa mada kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya Umoja wa Nchi za Afrika (AU).
Alisema kuwa kwa kipindi cha miaka 50 ya sasa katika nchi za Afrika hakuna uwiano kati ya walionancho na wasionacho na kwamba watu walionancho ni wachache ikilinganishwa na wasionacho.
Read more..
UWAKA watakiwa kuwaimarisha vijana kiimani
Na Ashura Kishimba
WANACHAMA wa Utume wa Wanaume Wakatoliki (UWAKA), wametakiwa kushiriki kikamilifu katika utume wao kwa Kanisa ili kuwawezesha vijana kuimarika kiimani.
Hayo yalibainishwa na Mwenyekiti wa Utume huo, Parokia ya Mtakatifu Petro Oysterbay, Cathree Theodory Abdallah wakati akizungumza na Tumaini Letu jijini Dar es Salaam kuhusiana na maendeleo ya umoja huo parokiani hapo, baada ya kupata uongozi mpya.
Read more..
Vijana mkimbilieni Mungu-Padri
Na Benedict Augustino
VJANA nchini wametakiwa kukimbilia msaada wa Mwenyezi Mungu katika kila jambo ili kupambana na vikwazo vya shetani.
Hayo yalibainishwa hivi karibuni na Paroko wa Parokia ya Yombo Kiwalani, Padri Efrahim Ogha wakati wa tafrija fupi ya kuwaapisha viongozi wa Kamati tendaji ya Vijana parokiani hapo.
Padri Ogha alisema kuwa watendaji hao wanatakiwa kutumia nyadhifa zao kumtumikia Mungu kwa sala na kazi.
Read more..
Rushwa yatia dosari uchaguzi Singida
Na Lilian Lihame,Singida
VITENDO vya rushwa vinavyodaiwa kufanyika kwenye uchaguzi mdogo wa vitongoji uliofanyika Mei 26, mwaka huu mkoani Singida, vimeelezwa kuchangia kuutia dosari uchaguzi huo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mkoa wa Singida, Wilfred Kitundu ameliambia Tumaini Letu kwamba vitendo vya rushwa vilivyokuwa vikifanywa na baadhi ya wagombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) vimechangia kwa kiasi kikubwa kukiangusha chama chake.
Alisema kuwa moja ya vitu hivyo ni pamoja na suala la utoaji wa fedha za kuendeleza miradi mbalimbali uliofanywa na CCM katika kampeni mbalimbali za uchaguzi huo.
Katika uchaguzi huo mdogo wa vitongoji CHADEMA iliachwa nyuma kwa kupata kiti kimoja katika ya viti 17 vilivyokuwa vikiwaniwa.
Read more...
Chama cha Wauguzi Wakatoliki chazinduliwa
Na Celina Joseph
WUGUZI nchini wametakiwa kuwahudumia wagonjwa kwa kuzingatia maadili ya kazi yao kwa kuwa Mwenyezi Mungu amewapatia karama ya kutunza na kulinda uhai.
Wito huo ulitolewa hivi karibuni na Mlezi wa Utume wa Familia Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kituo cha Msimbazi, Padri Novatus Mbaula, alipokuwa akizungumza kwenye uzinduzi wa Chama cha Wauguzi Wakatoliki Tanzania.
Padri Mbaula, alisema wauguzi wamekabidhiwa jukumu kubwa na Mwenyezi Mungu la kutunza na kulinda uhai wa maisha ya wagonjwa wanaowahudumia, kwa kujitahidi kuwa jirani mwema kwa wote wanaowahudumia bila kujali rangi, kabila, dini au itikadi.
Read more...
Mbinu za kufaulisha wanafunzi zaanikwa
Na Mary Yuda
ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, amesema kuwa mbinu pekee kwa ajili ya kuwezesha wanafunzi na shule mbalimbali kufanya vizuri zaidi ni kutegemea msaada wa Mungu.
Aidha Kardinali Pengo alitumia fursa hiyo kuwahimiza wamiliki wa shule mbalimbali nchini ikiwemo za Awali, Msingi na Sekondari pamoja na mambo mengine kujikita na kutegemea zaidi msaada wa Mungu kwa kwa kufanya hivyo shule zao zitapata mafanikio zaidi.
Read more...
Bunge ni chombo cha kutunga sheria
Na Mary Yuda
Bunge ni chombo cha kutunga sheria lakini pia naweza kusema ni moja kati ya Mihimili mitatu inayounda mfumo wa utawala kulingana na mfumo husika wa mgawanyiko wa madaraka, mihimili hiyo ni pamoja na Mahakama, Serikali na Bunge lenyewe.
Mfumo huu wa Bunge umerithiwa na nchi nyingi duniani kutoka nchini Uingereza , kama tunavyoshuhudia nchi mbalimbali duniani zikiwa na mfumo huu wa Bunge na kutokana na mfumo huu kutoka Nchini uingereza mara nyingi mara nyingi Bunge la Uingereza huitwa “Bunge mama au Mama wa Bunge” duniani.
Read More..
Habari za hapa na pale
HABARI ZA HAPA NA PALE
BRUSSELS 19.02.2013
Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Dakta DIODORUS KAMALA ameteuliwa na mabalozi wa nchi za Afrika kuwa Mwenyekiti wa Mabalozi hao.
Balozi KAMALA amepokea uenyekiti huo kutoka kwa Balozi wa Swaziland nchini humo JOEL NHELEKO aliyemaliza muda wake na kwamba Tanzania itashikilia nafasi hiyo katika kipindi cha miezi sita hadi Julai mosi mwaka huu.
Akizungumza mara baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo Balozi KAMALA mbali na kuelezea kufurahishwa na uteuzi huo, amesema kuwa atatumia fursa hiyo kuvutia fursa za kiuchumi kwa Tanzania.
Wakati huo huo, mabalozi wa nchi tano zinazozunguka Bonde la Ziwa Tanganyika, wamemchagua Balozi KAMALA kuwa mwenyekiti wao.
Nchi wanachama wa Bonde la Ziwa Tanganyika ni Burundi, Rwanda, Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na Zambia.
Dk Kamala, Brussels
VATICAN CITY 13.02.2013
Mkurugenzi wa Idara ya Habari ya Vatican, Padri FEDERICO LOMBARDI amesema kuwa licha ya kutangaza kujiuzulu, kwa sasa Baba Mtakatifu BENEDIKTO wa Kumi na Sita, anaendelea kuwa Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani.
Padri LOMBARDI ametoa ufafanuzi huo jana, alipokutana na waandishi wa habari mjini Vatican, waliotaka kuelewa majukumu ya Baba Mtakatifu baada ya kutangaza kuwa atajiuzulu ifikapo tarehe 28 ya mwezi huu.
Amewaambia waandishi hao wa habari kwamba, Baba Mtakatifu anaendelea na kazi zake hadi itakapofika tarehe aliyoitangaza ya kujiuzulu, Februari 28, akikalia Kiti cha Mtakatifu Petro.
Padri LOMBARDI amesema, kwa muda huu, hakutakuwa na mabadiliko yoyote katika ratiba ya Baba Mtakatifu ikiwemo kuongoza maadhimisho ya Kiliturjia ambayo ni pamoja na Misa ya Jumatano ya Majivu iliyoadhimishwa leo duniani kote.
Mjini Vatican, Misa hiyo ya Jumatano ya Majivu imefanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu PETRO, badala ya Kanisa la Mtakatifu SABINA kama ilivyo kawaida.
Amesema, pia kabla Kiti cha Mtakatifu Petro hakijawa wazi, Baba Mtakatifu atakutana na watu maarufu kutoka maeneo mbalimbali wakiwemo marais wa nchi za Romania na Guatemala na pia maaskofu wa Italia.
Juzi Jumatatu, Baba Mtakatifu BENEDIKTO wa Kumi na Sita aliyeanza kuliongoza Kanisa Katoliki tangu Aprili 19, 2005, alitangaza kuwa atajiuzulu kwa sababu ya umri mkubwa wa miaka themanini na tano {85}.
Martin Kuhanga {Zenit News}
VATICAN CITY 13.02.2013
Baba Mtakatifu BENEDIKTO wa Kumi na Sita ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza tangu alipotangaza kujiuzulu na kuwashukuru waamini kwa upendo wao na kumuombea.
Baba Mtakatifu, ametoa shukrani hizo leo mbele ya maelfu ya mahujaji waliokusanyika mjini Vatican kusali na kusikiliza mahubiri anayoyatoa kila wiki.
Akishangiliwa na mahujaji hao alipojitokeza, Baba Mtakatifu ameeleza kuwa ameamua kujiuzulu kwa Maslahi ya Kanisa akitambua kuwa uwezo wake kiroho na kimwili unapungua.
Juzi Baba Mtakatifu alitangaza kujiuzulu kuwa Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani ifikapo mwishoni mwa mwezi huu, Februari 28 kwa sababu ya umri mkubwa wa miaka themanini na tano {85}.
Baba Mtakatifu BENEDIKTO wa Kumi na Sita ameingia madarakani baada ya kufariki dunia kwa Mwenyeheri Baba Mtakatifu YOHANE PAULO wa Pili, Aprili mwaka 2005.
Hatua ya kujiuzulu kwa Baba Mtakatifu BENEDIKTO wa Kumi na Sita siyo ngeni Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani kwani imewahi kutokea hivyo zaidi ya miaka mia sita {600} iliyopita alipojiuzulu Papa GREGORY wa Pili mwaka 1415.
Martin Kuhanga (VATICAN RADIO)
DODOMA 13.02.2013
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais JAKAYA KIKWETE amekemea chokochoko za kidini na kuwataka waamini wa pande zote kuheshimiana.
Akizungumza mjini Dodoma, Rais KIKWETE amesema, chokochoko za kidini zinazojitokeza nchini zinatakiwa kukomeshwa kwani zinalifedhehesha Taifa.
Amesema, ili kulinda amani na utulivu uliopo nchini, waamini wa pande zote mbili wanatakiwa kuheshimiana na kuishi kwa upendo kwani chokochoko hizo zinaweza kuleta mapigano ambayo hayawezi kutufikisha popote.
Aidha, Rais KIKWETE amesema, amesikitishwa na mauaji yaliyotokea huko juzi mkoani Geita na kuongeza kuwa mapigano ya kidini hayajawaji kutokea nchini.Amesema, viongozi wa Dini wanao wajibu mkubwa wa kuhakikisha kuwa amani inaendelea kuwepo nchini kwani wanayo nafasi kubwa ya kufanya hivyo.
Liberatha Ruhikula {Habari Leo}
DAR ES SALAAM 13.02.2013
Waamini wametakiwa kuzidisha sala zao katika kuliombea Kanisa Katoliki ili liweze kudumu katika imani na kutangaza injili kwa ulimwengu wote.
Wito huo imetolewa na Padri kutoka Jimbo Katoliki la Masasi Padri LUKAS ACHINAMALINDI wakati akitoa katika mahubiri ya dominika katika Parokia ya Yombo Kiwalani Jimbo Kuu Katoliki la Dar es salaam.
Padri ACHINAMALINDI amesema kuwa katika Ulimwengu wa sasa uliogubikwa na changamoto mbalimbali waamini wanatakiwa kuzidisha sala ili Kanisa liweze kuendelea na utume wake ndani ya Tanzania na Ulimwengu kwa ujumla.
Amebainisha kuwa zipo changamoto mbalimbali zinazo hitaji sala ili ziweze kutatulika kwani akuna kinachoweza kushindikana katika sala.
Ameongeza kuwa kwa namna ya pekee waamini wanatakiwa kuwaombea viongozi wao wa kiroho ili waweze kuepukana na changamoto zinazoweza kuwakumba kwani nao wanaweza kuwa wadhaifu kama walivyo watu wengine.
Aidha amewataka waamini kuongeza bidii katika kulinda mali za kanisa ili kanisa liweza kuendeleza huduyma mbalimbali kutokana na mali hizo zilizopo.
Benedikto Agostino
DAR ES SALAAM 13.02.2013
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama POLYCARP Kardinali PENGO amewataka waamini wa Kanisa Katoliki nchini kupokea taarifa ya kujiuzulu kwa Baba Mtakatifu kwa moyo mkunjukufu.
Kardinali PENGO ametoa wito huo jana alipokutana na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam na kuwaasa waamini wa Kanisa Katoliki kuheshimu uamuzi huo wa Baba Mtakatifu.
Amesema, kuomba kupumzika kwa Baba Mtakatifu ni suala la unyenyekevu hivyo Wakatoliki wote wanatakiwa kuheshimu uamuzi wake kwa maslahi ya Kanisa lote ulimwenguni.
Kardinali PENGO amesema, Wakatoliki wanatakiwa kutambua kuwa suala la kujiuzulu kwa Baba Mtakatifu lipokelewe kama mpango wa Mungu wenye sababu maalum na siyo vinginevyo.
Kuhusu nani anaweza kuwa Baba Mtakatifu mpya, Kardinali PENGO amesema, nafasi ya uongozi katika Kanisa Katoliki hupangwa na Mungu na siyo kwa mapenzi ya mtu.
Liberatha Ruhikula( Mwananchi)
DAR ES SALAAM 07.02.2013
Imeelezwa kuwa uelewa mdogo wa sheria, maana na kutokuwepo kwa mifumo madhubuti ya kutoa taarifa za unyanysaji wa kijinsia vimechangia kuongezeka kwa matukio hayo.
Hayo yamebainishwa kwenye taarifa za awali kuhusu hali ya ukatili wa kijinsia uliofanyika katika wilaya 10 za Tanzania Bara na Zanzibar, na kuwasilishwa leo mbele ya waandishi wa habari na Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania-TAMWA,VALERIE MSOKA jijini Dar es salaam.
MSOKA amesema kuwa utafiti huo umeonesha kuwa asilimia 17 tu ya wananchi ndio wenye uelewa wa sheria za ukatili hali inayosababisha kutofuatilia haki zao wakati wa uvunjaji ma wakati mwingine kutoripotiwa kabisa kwa matukio hayo.
Amesema kuwa mila na desturi pamoja na utegemezi kiuchumi vimekuwa kikwazo cha kuripotiwa kwa baadhi ya matukio ya unyanysaji wa kijinsia na hivyo kushindwa kupatikana kwa takwimu sahihi za matukio hayo.
Ameongeza kuwa utafiti huo umebaini kuwa wananchi wanakosa majukwaa ya kukaa pamoja na kujadili changamoto zao na kwamba ni asilimia 13.5 tu ndiyo wanachama wa vyama vya kijamii.
MSOKA amezitaja wilaya 10 zitakazofaidika na mpango huo ni pamoja na Wete, Magharibi, Kusini Unguja, Kisarawe, Newala, Lindi vijijini, Mvomero, Kinondoni na Ilala.
Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania- TGNP, FESTA ANDREW MWANYINGILI, amesema kuwa utafiti huo utasaidia mashirika yanayojishughulisha na haki za kijinsia chini ya mradi wa Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wa Wanawake-GEWE kutoa elimu kwa umma
Editha Mayemba
HONIARA 07.02.2013
Mitikisiko imeendelea kwenye visiwa vya Solomon ikiwa ni siku moja mara baada ya visiwa hivyo kukumbwa na tetemeko la ardhi lililosababisha kutokea kwa Tsunami huku watu sita wakiuawa.
Wimbi lililokuwa na urefu wa mita moja lilivifunika vijiji kadhaa vilivyopo kwenye Kisiwa cha Santa Cruz kilichopo mashariki mwa bahari ya Pasific mara baada ya tetemeko hilo lililotokea mapema jana.
Nyumba kadhaa zimeathiriwa ama kubomolewa kabisa huku vijiji vitano vikiathiriwa na tetemeko hilo huku maafisa wa visiwa hivyo wakisema kuwa watu kadhaa wanadhaniwa kutojulikana mahali walipo.
Mitikisiko kadhaa imetokea mara baada ya kutokea kwa tetemeko hilo lililokuwa na kipimo cha nane nukta sifuri kwa vipimo vya matetemeko huku Idara ya Utafiti wa Jiolojia ya nchi hiyo ikisema kuwa tetemeko jingine limetokea leo asubuhi kwa kipimo cha sita nukta mbili.
Watu sita wakiwemo wazee watano na mtoto mmoja waliokuwa wamesombwa na maji wamethibitika kuwa wameuawa.
***
Fred Mosha, (Na msaada BBC News)
DODOMA 07.02.2013
Serikali imesema kuwa baadhi ya wanajeshi wanaotuhumiwa kuhusika kwenye makosa yanayohusiana na matumizi mabaya ya ofisi wamefikishwa mahakamani.
Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi PEREIRA AME SILIMA alipokuwa anajibu swali la nyongeza lililoulizwa na Mbunge wa Ubungo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, JOHN MNYIKA.
Akijibu swali hilo kwa niaba ya Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Naibu Waziri SILIMA ameliambia Bunge kuwa wanajeshi wanaotuhumiwa kuhusika na makosa hayo wamefikishwa Mahakamani na kwamba hakuna kinachofichwa katika tuhuma hizo.
Katika swali lake, MNYIKA alitaka kufahamu kile alichodai kuwa ni Serikali kuficha shughuli za biashara zinazodaiwa kufanyika kupitia vyombo vya ulinzi na usalama.
Awali akijibu swali la msingi lililoulizwa na Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM, MARTHA MLATA aliyetaka kufahamu sababu zinazoifanya Serikali kuweka wazi baadhi ya taarifa za ulinzi na usalama, Naibu Waziri SILIMA amesema kuwa kwa mujibu wa kanuni na sheria zinataka taarifa hizo zikiwemo za mapato na matumizi kuwasilishwa Bungeni kwa ajili ya kupitishwa.
Hata hivyo ameliambia Bunge kuwa ziko taarifa zingine za Jeshi zikiwemo za manunuzi ya silaha zitakazobakia kuwa siri.
***
Dino Mgunda